Thursday, November 2, 2017

TIMU YA TOTTENHAM YAIFANYIA KITU MBAYA REAL MADRID, MTANANGE WAMALIZIKA KWA 3-1. RONALDO HOI!Timu ya Tottenham imefuzu kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kutandaza soka safi na kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Real Madrid katika dimba la
Wembley.
Spurs, ikicheza ikiwa na nyota wake mshambuliaji Harry Kane ambaye amerejea uwanjani baada ya kupona maumivu ya paja, ilionyesha kiwango kizuri cha soka na alikuwa Dele Alli aliyefunga goli la kwanza katika dakika ya 27.

Dele Alli tena akaifungia Tottenham goli la pili katika kipindi cha pili kisha Christian Eriksen akafunga goli la tatu akiunganisha kwa utulivu krosi ya Kane, kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga goli pekee la Real Madrid.

Mshambuliaji Dele Alli akifunga goli la kwanza la Tottenham

Cristiano Ronaldo akiwa ameshika kiuona baada ya jahazi ya Real Madrid kuzama