Thursday, November 2, 2017

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MANCHESTER UNITED 2-0 BENFICA


Manchester United imeibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Benfica katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa kwenye dimba la Old Trafford.
Manchester United ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa Mile Svilar ambaye alijifunga na kisha kuongeza goli la pili kupitia penati iliyofungwa na Daley Blind.

Katika mchezo huo Manchester United pia ilikosa penati moja iliyopigwa na Anthony Martial iliyopatikana baada ya beki kuunawa mpira.


Romelu Lukaku akijiandaa kupiga penati lakini kocha Jose Mourinho akatoa maagizo apige Daley Blind

Daley Blind akipiga penati na kufunga goli la pili la Manchester United