Thursday, December 21, 2017

ARSENAL YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA CARABAO KWA KUIFUNGA WEST HAM BAO 1-0


Kocha Arsene Wenger amesema Arsenal haipaswi kupata majeruhi zaidi katika kipindi hiki cha michezo mingi baada ya Olivier Giroud kuumia misuli wakishinda goli 1-0 dhidi ya West Ham.

Wenger, ambaye alifanya mabadiliko ya wachezaji 11 katika kikosi chake akijipanga kuwavaa Newcastle jumamosi, alipata wakati mgumu kuipenya ngome ya wageni wao.
Lakini mshambuliaji wa Uingereza Danny Welbeck alifanikiwa kuipenya ngome ya West Hama kabla ya mapumziko akitumbukiza kimiani mpira wa krosi ya Mathieu Debuchy.


Danny Welbeck akifuga goli pekee katika mchezo huo wa kombe la Carabao

Kipa wa West Ham Joe Hart akiwa chini huku mpira ukiwa umetinga kwenye wavu wake