Sunday, December 17, 2017

CHELSEA NA ARSENAL ZASHINDA LIGI KUU ENGLAND, CONTE APAGAWISHWA NA REKODI ZA MAN CITY


Kocha wa Chelsea Antonio Conte amesema kiwango cha timu yake kimesahaulika kutokana na rekoni inazovunja Manchester City, kauli aliyoitoa baada ya Chelsea kuifunga Southampton goli 1-0, na kushinda michezo nane kati ya kumi ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Goli pekee la ushindi katika mchezo huo lilifungwa na Marcos Alonso kwa shuti zuri na kuifanya Chelsea kufikisha pointi sawa na Manchester United iliyokatika nafasi ya pili ambayo inashuka dimbani leo dhidi ya West Brom.


Kipa wa Southampton akiruka bila mafanikio kuufuata mpira uliopigwa na Marcos Alonso

Kocha wa Newcastle Rafael Benitez amesema anahitaji kufanya kitu Januari, baada ya kuporomoka katika nafasi ya kushuka daraja baada ya jana kufungwa goli 1-0 na Arsenal.

Arsenal ilipata ushindi huo kupitia goli zuri la Mesut Ozil katika kipindi cha kwanza na lilitosha kabisa kwa kikosi cha Arsene Wenger kuibuka na ushindi.


Mjerumani Mesut Ozil akiachia shuti na kufunga goli pekee la Arsenal katika mchezo huo