Sunday, December 31, 2017

CHELSEA YAFUNGA MWAKA 2017 KWA KWA KUINYUKA STOKE CITY BAO 5-0, WAPANDA NAFASI YA PILI

Timu ya Chelsea imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya hii leo kuibuka na ushindi wa kishindo wa magoli 5-0 dhidi ya Stoke City na kumaliza mwaka 2017 kwa ushindi.
Katika mchezo huo wenyeji Chelsea walifunga goli la kwanza kupitia kwa Antonio Rudige kufuatia krosi ya Mbrazil Willian kisha baadaye Danny Drinkiwater akaongeza goli la pili kisha Pedro akafunga la tatu.
Willian aliongeza goli la nne kwa mkwaju wa penati baada ya kuchezewa rafu na Geoff Cameron na katika dakika ya 88 Zappacosta akakamilisha karamu ya magoli kwa kufunga goli lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza.
Antonio Rudige akifunga goli la kwanza la Chelsea katika mchezo huo

Danny Drinkwater akifunga kwa shuti la kuubetua mpira kwenye kona ya goli.