Thursday, December 21, 2017

CHELSEA YATINGA NUSU FAINALI YA KOMBE LA CARABAO


Alvaro Morata amefunga goli la dakika za majeruhi na kuifanya Chelsea kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Carabao kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Bournemouth.
Willian alifunga goli la kwanza kufuatia shambulizi nzuri ambalo liliishia kwa Cesc Fabregas kutoa pasi ya mwisho kwa Willian.

Bournemouth ilifikiria kuwa mchezo huo ungeingia katika dakika za ziada baada ya Dan Gosling kufunga goli la kusawazisha lakini Morata aliyetokea benchi akaongeza la pili.


Dan Gosling akifunga goli la kusawazisha hata hivyo Chelsea waliongeza goli la ushindi baadaye.

Mshambuliaji Alvaro Morata aliyetokea benchi akifunga goli la ushindi la Chelsea