Wednesday, December 27, 2017

CONTE ASEMA KUKOSA BAHATI KUMEWAFANYA WASHINDWE KUWAFIKIA MAN CITY, MAN UNITED SARE TENA!

Kocha Antonio Conte amesema ni kukosa bahati tu kulioifanya timu yake wa Chelsea kuwa pointi 13 nyuma ya vinara wa ligi Manchester City baada ya kuifunga Brighton 2-0.
Chelsea imepata ushindi wa sita mfululizo katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya jana kusakata kandanda safi na kupata magoli hayo kupitia kwa Alvaro Morata na Marcos Alonso.

Alvaro Morata akifunga kwa mpira wa kichwa goli la kwanza la Chelsea
Shuti la Jesse Lingard limeinyima Burnley kupata ushindi katika dimba la Old Trafford na kutoka sare ya magoli 2-2 matokeo ambayo yanafifisha matumaini ya kukimbiza ubingwa.

Katika mchezo huo Ashley Barnes aliwafungia wageni goli la kwanza na kisha baadaye Steven Defour akafunga goli la pili na kufanya hadi mapumziko matokeo kuwa 2-0.
Jesse Lingard akiachia shuti na kuisaidia Manchester United kulazimisha sare dhidi ya Burnley