Tuesday, December 12, 2017

DIEGO MARADONA AZINDUA SANAMU YAKE INDIA

Nyota mkongwe wa soka duniani Diego Maradona ametambulisha sanamu yake akiwa ameshikilia kombe la dunia nchini India.
Mchezaji huyo anayeheshimika katika mji wa Kolkata ametambulisha sanamu hiyo baada ya kuhairisha mara kadhaa shughuli hiyo.
Katika hafla hiyo Maradona amesisitiza kwa masahabiki hao wa India wanaomhusudu mno kuwa yeye si Mungu bali ni mchezaji soka tu.
Mbali na uzinduzi wa sanamu Maradona alitoa hundi kwa wagonjwa 11 wa saratani pamoja na kukabidhi gari la wagonjwa.
Sanamu ya Diego Maradona iliyozinduliwa mjini Kolkata nchini India
Nyota mkongwe wa soka Diego Maradona akiweka saini yake kwenye mpira