Thursday, December 14, 2017

EPL: LUKAKU AONDOA UKAME WA MAGOLI AKIIFUNGIA BAO PEKEE MAN UNITED USIKU DHIDI YA BOURNEMOUTH

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa angekuwa kwenye mapumziko nchini Brazil ama Los Angeles iwapo angekuwa anafikiri mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza zimeisha.
Mourinho ametoa kauli hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Bournemouth, goli lililofungwa na mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku kwa mpira wa kichwa kufuatia krosi ya Juan Mata.
Romelu Lukakku akiangalia mpira alioupiga kwa kichwa ukielekea kutinga wavuni kwenye kona ya juu ya goli

Romelu Lukaku (katikati kushoto) akipongezwa baada ya kuziona nyavu za Bournemouth
Lukaku akiruka kufunga bao


Scott McTominay (kulia)
Phil Jones (kulia) akichuana vikali na Callum Wilson

Jesse Lingard akijaribu kupiga mpira kwa aina yake mbele ya wachezaji wa Bournemouth
Charlie Daniels akipiga shuti kali
Nahodha wa Bournemouth akiwa hoi baada ya kushindwa kutumia nafasi kuifungia bao timu yake