Sunday, December 31, 2017

FULL TIME: CRYSTAL PALACE 0-0 MANCHESTER CITY

Baada ya kushinda michezo 18 mfululizo ya Ligi Kuu ya Uingereza, hatimaye Crystal Palace imefanikiwa kusimamisha rekodi ya ushindi wa Manchester City hii leo.
Crystal Palace licha ya kutoa sare tasa na vinara wa ligi Manchester City, pia ingeweza kuibuka na ushindi wa goli moja lakini kipa Enderson aliwanyima ushindi. 


Palace walidhani kuwa wataibuka na ushindi baada ya kupata penati dakika za mwisho baada ya kuangushwa Wilfred Zaha lakini penati ya Luka Milivojevic ilipanguliwa.
Licha ya kutibuliwa rekodi ya ushindi mfululizo Manchester City pia imejikuta ikikumbwa na hofu ya majeruhi baada ya Kevin De Bruyne na Gabriel Jesus kuumia.
Raheem Sterling akimuangusha katika eneo hatari Wilfred Zaha na muamuzi kuamua mkwaju wa penati
Luka Milivojevic akishuhudia mpira wa penati aliyoipiga ukizuiliwa kwa miguu na kipa Enderson wa Manchester City