Sunday, December 3, 2017

HAZARD ATUPIA MBILI CHELSEA IKIIBUKA NA USHINDI WA BAO 2-1 DHIDI YA NEWCASTLE UNITED


Eden Hazard amefunga mara mbili wakati Chelsea ikitandaza soka safi na kuifunga Newcastle na kufikia pointi sawa na Manchester United ambao wanavaana na Arsenal.
Hazard aliifungia Chelsea goli la kusawazisha akirejea katika kikosi cha kwanza baada ya Dwight Gayle kuipatia Newcastle goli la kuongoza la kushtukiza lililowaamsha Chelsea.

Mshambuliaji Alvaro Morata alifanya matokea kuwa magoli 2-1 baada ya kufunga kwa mpira wa kichwa kufuatia krosi ya Victor Moses, Hazard akafunga la tatu kwa penati.


Eden Hazard akijipinda na kuachia shuti lililozaa goli la kusawazisha la Chelsea

Alvaro Morata akipiga mpira kwa kichwa na kufunga goli la pili la Chelsea