Friday, December 29, 2017

KOCHA ARSENE WENGER HANA WASIWASI YA KUMKOSA SANCHEZ ANAYEONDOKA JANUARI, WASHINDA BAO 3-2 DHIDI CRYSTAL PALACE.


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema kuwa hana wasiwasi wa kumpoteza Alexis Sanchez Januari licha ya mshambuliaji huyo kufunga mara mbili wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Crystal Palace.
Crystal Palace ilisawazisha goli kupitia kwa Andros Townsend baada ya Shkodran Mustafi kufunga goli la kwanza katika mchezo huo na kisha baadaye katika kipindi cha pili akafunga mawili kwa muda wa dakika nne.
Crystal Palece ilipata goli la pili katika kupitia kwa James Tomkins kwa mpira wa kichwa, hata hivyo walishidwa kusawazisha la tatu na kuifanya Arsenal iliyokatika nafasi ya sita kuwa na pinti sawa na Tottenham iliyonafasi ya tano.
Mchezaji wa Arsenal Shkodran Mustafi akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Mshambuliaji Andros Townsend akifunga goli la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 1-1
Alexis Sanchez akifunga goli lake la pili katika mchezo huo na kufanya matokeo kuwa 3-2