Sunday, December 3, 2017

KOCHA SAM ALLARDYCE AANZA KWA USHINDI AKIWA NA EVERTON, BAO 4-0

Kocha Sam Allardyce ameanza kuinoa Everton kwa ushindi wakati Gylfi Sigurdsson na Dominic Calvert-Lewin wakifunga magoli katika kupindi cha pili na kuizamisha Huddersfield.

Allardyce, aliyeteuliwa kuinoa timu hiyo kwa mkataba wa miezi 18 siku ya Alhamis, ameshuhudia kikosi chake kikionyesha uimara hii leo licha ya kutokuwa na kiwango bora cha kutandaza soka.
Kocha Sam Allardyce akinyoosha mkono juu kuashiria mambo safi baada ya ushindi
Katika mchezo mwingine Demarai Gray alifunga goli pekee la ushindi la Leicester City kufuatia krosi Riyad Mahrez na kukosa nafasi ya kufunga goli la pili katika kipindi cha pili wakizamisha Burnley.