Monday, December 18, 2017

LA LIGA: BARCELONA 4-0 DEPORTIVO, LUIS SUAREZ, PAULINHO WAIBEBA BARCELONA


Luis Suarez amefunga goli lake la nane na la tisa la ligi katika msimu huu wakati Barcelona ikishinda magoli 4-0 dhidi ya Deportivo, na angepata hat-trick iwapo ingetumika teknolojia ya kuaini mpira uliokatiza mstari wa goli.

Suarez alifunga goli la kwanza katika kipindi cha kwanza kabla ya Mbrazil Paulinho kuongeza goli la pili katika dakika ya 41. Baada ya mapunziko Suarez aliongea goli lake la pili na kisha baadaye Paulinho tena akafunga goli la nne.


Mshambuliaji nyota wa Barcelona Luis Suarez akifunga goli huku Lionel Messi akiangali

Luis Suarez akiupiga kimanjonjo mpira ambao ulivuka mstari wa goli lakini goli hilo likakataliwa