Sunday, December 31, 2017

LIVERPOOL 2 vs 1 LEICESTER CITY, MOHAMED SALAH AIBEBA LIVERPOOL NYUMBANI!


Raia wa Misri Mohamed Salah amefunga magoli mawili na kuisaidia Liverpool kuongeza rekodi yao ya kutofungwa katika michezo 15 kwenye michuano yote baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Leicester City.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Anfield Jamie Vardy aliwapatia wageni goli la kuongoza akiitumbukiza kiulani pasi ya Riyad Mahrez goli lililoduma hadi kipindi cha pili pale Salah alipoisawazishia Liverpool.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri baadaye tena alimzungusha Harry Maguire na kuachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli la pili na kufikisha magoli 17 katika michezo ya Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu huu.


Mshambuliaji nyota wa Leicester City akifunga goli la kwanza katika mchezo huo

Mshambuliaji nyota wa Liverpool Mohamed Salah akifunga goli la kusawazisha kabla ya baadaye kuongeza la pili