Tuesday, December 12, 2017

MAN U YAFUNGWA NA MAN CITY BAO 2-1, JOSE AMTUPIA LAWAMA REFA KUWANYIMA PENATI


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema matumaini ya kikosi chake katika mbio za ushindi ni kama yametoweka baada ya refa Michael Oliver kuwanyima penati wakati wakipoteza kwa magoli 2-1 dhidi ya Manchester City.
Kwa matokeo hayo kikosi hicho cha Pep Guardiola kinaongoza Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi 11 na Manchester City kuwa timu ya kwanza kushinda michezo 14 mfululizo katika msimu mmoja.
Katika mchezo huo wageni Manchester City walikuwa wakwanza kufunga goli kupitia mchezaji bora wa mchezo huo David silva, lakini makosa ya beki Nicolas Otamendi yalimfanya Marcus Rashford asawazishe, hata hivyo Otamendi akaongeza goli la pili na kufuta makosa yake.


Mchezaji David Silva akifunga goli la kwanza katika mchezo huo

Marcus Rashford akiachia shuti na kufunga goli pekee la Manchester United