Sunday, December 3, 2017

MAN UNITED YAIPA KIPIGO ARSENAL CHA BAO 3-1, MASHABIKI WAMZOMEA WENGER! POGBA AONESHWA KADI NYEKUNDU!

Timu ya Manchester United imevunja mwiko wa Arsenal kutofungwa nyumbani kwao katika msimu huu tangu Januari mwaka huu baada ya kuitundika magoli 3-1 katika dimba la Emirates.
Katika mchezo huo Antonio Valencia alikuwa wa kwanza kufunga goli baada ya kunasa pasi isiyonamacho ya Laurent Koscielny na kupachika goli kwa mpira uliompita tobo kipa wa Arsenal.
Jesse Lingard alifunga goli la pili baada ya kugongeana vyema na Romelu Lukaku na Anthony Martial, Alexandre Lacazette akaifungia Arsenal goli kisha Lingard akatupia la tatu.
Antonio Valencia akifunga goli kwa shuti kali lililompita tobo kipa wa Arsenal Petr Cech
Alexandre Lacazette akifunga goli pekee la Arsenal katika mchezo huo baada ya mabeki wa Manchester United kudhani ameotea