Thursday, December 21, 2017

MANCHESTER CITY KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA CARABAO KWA MIKWAJU YA PENATI 4-3 DHIDI YA LEICESTER CITY.


Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema anafuraha mno baada ya kikosi chake kutinga kwa ushindi wa matuta 4-3 nusu fainali ya kombe la Carabao Cup dhidi ya Leicester City.

Kipa Claudio Bravo aliyeokoa mikwaju miwili ya penati dhidi ya Wolves katika raundi iliyopita jana pia alipangua penati ya Riyad Mahrez na Jamie Vardy penati yake kugonga mwamba.

Wenyeji ilibidi waende hadi dakika za lala salama ili kukomboa goli moja walilofungwa na Bernardo Silva, na alikuwa Jamie Vardy aliyesawazisha goli kwa mkwaju wa penati.


Mshambuliaji Jamie Vardy akifunga mkwaju wa penati uliofanya mchezo huo uende katika muda wa nyongeza na kuishia kwa matuta

Kipa wa Manchester City Claudio Bravo akipangua penati ya Riyad Mahrez