Thursday, December 14, 2017

MANCHESTER CITY YAIFUNGA BAO 4-0 SWANSE CITY

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amepongeza ari ya kushinda ya 'Mnyama' David Silva baada ya magoli yake kuisaidia kuichakaza Swansea kwa magoli 4-0, na kuendeleza ushindi kwa michezo 15 mfululizo.
Silva alifunga magoli mawili na kisha Kevin de Bruyne alifunga moja na Sergio Aguero aliihakikishia Manchester City kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 11, huku Swansea ikibakia mkiani mwa Ligi hiyo.
David Silva 'Mnyama' akifunga goli la kwanza kwa kuugonga kiaina mpira
Beki wa Leicester City, Harry Maguire, amesema kujiamni kwao kunazidi kuimarika chini ya kocha Claude Puel baada ya kupata ushindi wa kiurahisi wa magoli 4-1 dhidi ya Southampton.

Puel alitimuliwa na Southmpton mwezi Juni, baada ya kuinoa kwa msimu mmoja na kuisaidia kushika nafasi ya nane na kuifikisha fainali ya Kombe la Ligi.
Riyad Mahrez akifunga goli la kwanza la Leicester City katika mchezo huo