Friday, December 15, 2017

MANCHESTER UNITED: BEKI ERICK BAILLY KUFANYIWA UPASUAJI

Related image
Haki miliki ya picha Rex Features Image caption Eric Bailly alikuwa mchezaji wa kwanza kununuliwa na Mourinho alipojiunga na Manchester United
Beki wa Manchester United Eric Bailly huenda akahitaji kufanyiwa upasuaji zaidi kwenye jeraha "mbaya" la kifundo cha mguu, anasema meneja Jose Mourinho.
Mourinho amesema beki huyo wa kati wa miaka 23 ambaye aliumia akichezea Ivory Coast.
Hajachezea United tangu walipolazwa na Chelsea mnamo 5 Novemba.
Hata hivyo, anatarajiwa kurejea kabla ya msimu kumalizika.

"Sitaki kuwa mtu wa kuonesha kutokuwa na matumaini. Namwachia madaktari.

"Tunajaribu kutumia matibabu kwa kipimo, lakini hilo lisipofanikiwa, labda atahitaji kufanyiwa upasuaji lakini hebu tusubiri muda kidogo.

Mourinho hata hivyo amesema amefurahishwa na kurudi kwa mabeki wengine Chris Smalling na Phil Jones ambao walianza kwenye mechi ya Jumatano ambayo walishindwa Bournemouth 1-0.
Bailly alikuwa mchezaji wa kwanza kujiuna na United baada ya Mourinho kuteuliwa meneja.
Alijiunga nao kutoka Villarreal mwaka 2016 kwa £30m.