Monday, December 18, 2017

MANCHESTER UNITED WAENDELEZA USHINDI TENA...WAIFUNGA BAO 2-1 WEST BROM


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameapa kuwa kikosi chake kitapambana hadi mechi ya mwisho, baada ya kuifunga West Brom Magoli 2-1 na kuwa pointi 11 nyuma ya vinara wa ligi Manchester City.
Katika mchezo huo Romelu Lukaku alikuwa wa kwanza kufumania nyavu kwa mpira wa kichwa akiunganisha krosi ya Marcus Rashford, likiwa ni goli lake la pili katika michezo miwili mfululizo baada ya kuondoa gundu la kutofunga kwa muda.

Kinda Jesse Lingard aliongeza goli la pili kabla ya mapumziko kwa shuti lililomgonga Ahmed Hegazi na kumpoteza mahesabu kipa wa West Brom. Gareth Barry aliifungia West Brom goli pekee la kufutia machozi.


Mshambuliaji Romelu Lukaku akiruka juu na kufunga goli kwa mpira wa kichwa

Jesse Lingard akifunga goli kwa shuti lililomgonga beki wa West Brom Ahmed Hegazi