Monday, December 25, 2017

ROBERTO FIRMINO AIOKOA LIVERPOOL DAKIKA ZA MWISHO NA KUTOKA SARE NA ARSENALYA GOLI 3-3


Goli la shuti kali la Roberto Firmino limeisaidia Liverpool kutoa sare katika mchezo mzuri wa Ligi Kuu ya Uingereza ulioshuhudia Arsenal ikifunga magoli matatu ndani ya dakika tano za kipindi cha pili.
Arsenal ilikuwa nyuma kwa magoli 2-0 yaliyofungwa na Philippe Coutinho aliyefunga goli la kwanza kwa mpira wa kichwa kabla ya raia wa Misri Mohamed Salah kuongeza goli la pili katika kipindi cha pili.
Lakini hafla Arsenal walizinduka na kufunga goli la kwanza kupitia kwa Alexis Sanchez akifunga kwa mpira wa kichwa krosi ya Hector Bellerin, kabla ya Granit Xhaka kutumbukiza la pili kisha Mesuit Ozil kufunga la tatu.


Philippe Coutinho akifunga goli kwa mpira wa kichwa hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kufunga goli kwa mpira wa kichwa katika Ligi Kuu ya Uingereza

Mohamed Salah akifunga goli la pili la Liverpool kwa shuti lililomshinda kipa wa Arsenal

Alexis Sanchez akiifungia Arsenal goli la kwanza lililoamsha ari ya kusawazisha magoli waliyofungwa na kuongeza moja

Roberto Firmino akiisawazishia Liverpool goli la tatu na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya magoli 3-3