Sunday, December 17, 2017

RONALDO AISAIDIA REAL MADRID KUTETEA KOMBE LA DUNIA

Cristiano Ronaldo amefunga goli la ushindi kwa mkwaju wa mpira wa adhabu wakati Real Madrid ikiweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kutetea Kombe la Dunia kwa vilabu baada ya kuifunga Gremio ya Brazil goli moja bila.
Ronaldo aliyeshinda tuzo ya Ballon d’Or mwezi huu na kujitangaza kuwa ni mchezaji bora katika historia, huku baadhi ya watu wakimbeza, lakini inaonekana anaendelea kuziba midomo wanaompinga kwa kutwaa makombe.

Kwa goli hilo la Ronaldo, 32, linamfanya kufikisha magoli 7 katika michuano hiyo sawa na mfalme wa soko duniani Pele aliyefunga idadi kama hiyo ya magoli katika michuano hiyo wakati huo ikijulikana kama kombe la mataifa.
Cristiano Ronaldo akipiga mpira wa adhabu ulioipatia ushindi Real Madrid na kutwa kombe la dunia
Kipa wa Gremio akiruka bila ya mafanikio kuufuata mpira wa adhabu uliopigwa na Ronaldo