Sunday, December 3, 2017

TIMU YA LIVERPOOL YAENDELEZA KUTOA DOZI NONO UGENINI, YAIBAMIZA BAO 5-1 BRIGHTON


Timu ya Liverpool imeendeleza ubabe wake wa kufumania nyavu ugenini kwa kuitundika magoli 5-1 Brighton na kukwea hadi katika nafasi nne za juu za Ligi Kuu ya Uingereza.
Alikuwa Emre Can alifunga goli la kwanza kwa kichwa kufuatia mpira wa kona ya Philippe Coutinho kisha Roberto Firmino akaongeza la pili na la tatu.

Glenn Murray aliyepoteza nafasi mbili za kufunga, akafunga goli kwa mkwaju wa penati, uliomshinda kipa Simon Mignolet. Countinho alifunga la nne na Dunk kujifunga.


Emre Can akiwa amefunga goli na kuiacha safu ya ulinzi ya Brighton ikilaumiana

Roberto Firmino akifunga goli la tatu la Liverpool na la pili kwake katika mchezo huo