Friday, December 29, 2017

WASANII ASLAY NA NANDY WATUA BUKOBA LEO HII, TAYARI KWA SHOW YA MIAKA 9 YA KASIBANTE REDIO KWENYE UKUMBI WA ST. THEREZA KESHO 30/12/2017

Wasanii wa Muziki wa Bongo Flava, Aslay (Katikati) (kulia ni Nandy na kushoto ni Chiba muda mfupi baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege Mjini Bukoba.
Kesho Jumamosi wanatarajiakuangusha bonge la show kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba pale ukumbi wa St.Theresa karibu na banki ya NMB.
Show hiyo ni moja ya maadhimisho ya miaka 9 ya uwepo wa Kasibante Fm Radio Bukoba tangu kuanzishwa kwake.
Show hiyo itaanza majira ya saa moja jioni hadi majogoo huku Wheel Steel ikisimamiwa na DJ`s kutoka Pro24Tanzania.
Mmiliki wa www.bukobasports.com Faustine Ruta (kulia) akiwa na Aslay (kushoto).


Msanii Nandy (kushoto) akiwa na Faustine Ruta

Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Redio Kasibante FM 88.5 wakiwa picha ya pamoja.
Msanii Aslay akiwa kwenye P.A kwenye Viunga vya Bukoba leo hii.

Baadhi wa Wananchi wa Mwaloni wakishangaa wasanii hao wakati wanapita eneo hilo huku wakiacha kufanya kazi zao za Dagaa katika eneo hilo na kuwatupia macho
Wakishangaa kwa Muda.