Monday, January 8, 2018

ARSENAL YACHAPWA BAO 4-2 WAKATI KOCHA WAO WENGER AKITUMIKIA ADHABU YA FA. WATUPWA NJE!


Arsenal ikicheza huku ikishuhudiwa na kocha wake Arsene Wenger ambaye anatumikia adhabu ya FA ya kutoongoza kikosi hicho, imepata kipigo cha magoli 4-2 kutoka kwa Nottingham Forest na kutolewa katika kombe la FA.
Wenger could only watch from the stands after beginning a three-match touchline ban Wenyeji Nottingham walipata goli la kwanza kupitia kwa Eric Lichaj kwa mpira wa kichwa lakini goli hilo lilidumu kwa dakika tatu tu na kusawazishwa na Per Mertesacker akiuwahi mpira wa kichwa wa Rob Holding uliogonga mwamba.
Lichaj akaongeza goli la pili kwa Nottingham inayonolewa na kocha Gary Brazil, akifunga vizuri goli kwa shuti la mpira wa kunyanyua juu. Ben Brereton akaiongeza la tatu kwa mpira wa penati huku Danny Welbeck akiifungia Arsenal goli la pili, Kieran Dowell akafunga la nne.


Eric Lichaj akiifungia Nottingham Forest goli la kwanza kwa mpira wa kichwa

Ben Brereton akiwa amepiga mpira wa penati na kujaa wavuni huku kipa wa Arsenal akipotea mahesabu.Wenger wouldn't comment on  the fact Kieran Dowell appeared to kick the ball twice