Sunday, January 21, 2018

DORTIMUND: HAKUNA MAZUNGUMZO YA KUMUUZA AUBAMEYANG

Image result for Pierre-Emerick AubameyangKOCHA wa Borussia Dortmund Peter Stoger anasema kuwa hakuna ombi la kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang lililowasilishwa na Arsenal.
Mshambuliaji huyo wa Gabon ambaye ananyatiwa na the Gunners, hakusafiri na wachezaji wenzake kwa mechi ya Ijumaa dhidi ya Hertha berlin ambayo ilikamilika 1-1.
"hakuna mazungumzo yoyote katika meza kuhusu uhamisho wa Aubameyang ,yanayoendelea ni uvumi. alisema Stoger.
"Tunapanga na Pierre-Emerick Aubameyang na kuna vile atakavyorudi katia kikosi cha kwanza cha timu ."
Aubameyang pia alikosa mechi ya Jumapili iliotoka sare ya 0-0 dhidi ya Wolfsburg baada ya kukosa kuhudhuria mkutanoi wa timu.