Saturday, January 6, 2018

FA CUP: MAN UNITED 2-1 DERBY, JESSE LINGARD NA LUKAKU WAKIOKOA JAHAZI OLD TRAFFORD UNITED WAKIIBUKA NA USHINDI!


Romelu Lukaku (katikati) na Jesse Lingard (kulia) ndio waliokuwa mwiba kwa Timu ya Derby kila mmoja akiifungia bao moja moja  Manchester United katika dakika za mwisho na kufanikisha kuivusha hatua inayofuata Timu hiyo kwenye Ligi ya  FA Cup jana usiku. Ligi hiyo inaendelea tena hii leo.

Lingard akishangilia bao lake kwa kuifunga Timu ya  Derby na Man United kumaliza mtanange huo kwa bao 2-0.

Lukaku akipongezwa mara baada ya kuifungia bao la pili Man United na kuivusha hatua ya raundi ya Nnne ya  FA Cup
Marcus Rashford chupuchupu na mara kadhaa alikuwa anajaribu kuifunga Timu hiyo huku mashuti yake mengi yakigonga posti mara kwa mara.

Rashford shuti lake hapa liligonga posti

Scott Carson kipa wa Derby alikomaa langoni mwake na kuweza kuilinda Timu yake kisawasawa lakini dakika ya mwishoni maji yalizidi.

Paul Pogba pia alifanya juhudi kubwa katika mechi hiyo lakini bahati hakuwa nayo katika mtanange huo.

Romelu Lukaku chupuchupu akisikitika baada ya kukosa nafasi 

George Thorne (kati kushoto) na Huddlestone (kati kulia) wakiwa wanaangalia mpira kwa makini huku Pogba na Rashford wakiwaweka Mtu kati!

Sergio Romero mlinda lango namba mbili ndiye aliyekuwa langoni
Pogba akifanya yake