Monday, January 22, 2018

FULL TIME: KAGERA SUGAR 0 vs 2 SIMBA SC, NDEMLA NA BOCCO WALIPA KISASI KAITABA LEO, SIMBA AREJEA KILELENI!

Na Faustine Ruta, Bukoba
Simba imezidi kujichimbia kileleni baada ya kuichapa Kagera Sugar kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba hii leo jioni.

Bao za Simba Sc leo hii zimefungwa kipindi cha pili baada ya kumaliza dakika 45 timu zote mbili zikiwa 0-0. Bao la kwanza limefungwa na Said Ndemla na bao la pili limefungwa na John Bocco baada ya mabeki wa Kagera Sugar kujichanganya.
Kipindi cha pili dakika ya 70 Said Ndemla aliipatia Simba goli la Kwanza na kufanya Simba kuongoza kwa bao 1-0. Wakati huo baaada ya bao hilo Shomari Kapombe aliingia kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe Simba akichukua namba ya Gyan.  

Kipindi hicho cha pili dakika ya 80 John Bocco aliipachikia Simba bao la pili Baada ya kazi nzuri ya Shomari Kapombe aliyeingia kipindi hicho cha pili na Simba kuwatandika bao la pili na Simba kuongoza bao 2-0' Hadi dakika 90 zinamalizika Simba 2-0 Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Ushindi huo unawarudisha Simba kileleni wakiwa na pointi 32.

Kiungo wa Simba Hamis Said Juma (Ndemla) akipeta baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya timu ya Kagera Sugar. Picha zote na Faustine Ruta
Mara baada ya Mchezo huo kumalizika Msemaji wa klabu ya Simba Sports Club, Haji Manara ambaye ameshuhudia mchezo huu Mbashara akiwa  jukwaa kuu ameipongeza Timu ya Kagera Sugar japo pamoja na kupoteza mchezo huo amesema waendelee hivyo hivyo ili waweze kuumaliza msimu huu wakiwa nafasi za juu kama msimu uliopita. hapo hapo ameimwagia sifa kemukemu Timu yake Simba kwa kurejea kileleni.

Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar kilichoanza dhidi ya Timu ya Simba SC hii leo kwenye Dimba la Kaitaba mjini Bukoba jioni hii kwenye Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara. 
Kikosi cha Simba kilichoanza dhidi ya Timu Kagera Sugar.  
Mwamuzi akiwa na Manahodha wa Timu zote mbili Kagera Sugar vs Simba Sc muda mfupi kabla ya Mechi kuanza, akiwaonesha ni yupi anafunga huku na yupi anafunga kule. Picha zote na Faustine Ruta Nohodha wa Timu ya Simba John  Bocco(kulia) akielezwa jombo na Mwamuzi.
Picha ya pamoja
Timu zote mbili zikisalimiana kabla ya mtanange kuanza.
Wachezaji wakimsikiza Mgeni ramsi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu muda mfupi kabla ya mtanange kuanza.
Wachezaji wa Timu ya Simba Sc wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi wakati anawapa neno kabla ya mtanange kuanza. 
Wachezaji wa Timu ya Kagera Sugar nayo wakimsikiza kwa Makini.
Wachezaji wa Akiba wa Timu ya Kagera Sugar wakiwatazama wenzao uwanjani hii leo kwenye Dimba la Kaitaba mjini Bukoba.
Msemaji wa klabu ya Simba Sports Club, Haji Manara akiutazama mchezo huo akiwa meza kuu sambamba na mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu na Viongozi wengine.
Raia wa Kigeni nao walikuwa macho Kaitaba kuucheki mchezo huo uliokuwa wa kukata na Shoka ambao Simba wameitafuna Miwa ya Kagera Sugar.
Kipindi cha pili dakika ya 70 Said Ndemla aliipatia Simba goli la Kwanza na kufanya Simba kuongoza kwa bao 1-0. Wakati huo baaada ya bao hilo Shomari Kapombe aliingia kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe Simba akichukua namba ya Gyan.
Kipindi hicho cha pili dakika ya 80 John Bocco aliipachikia Simba bao la pili Baada ya kazi nzuri ya Shomari Kapombe aliyeingia kipindi hicho cha pili na Simba kuwatandika bao la pili na Simba kuongoza bao 2-0' Hadi dakika 90 zinamalizika Simba 2-0 Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Ushindi huo unawarudisha Simba kileleni wakiwa na pointi 32.
Kapombe akipongezana na mshambiliaji wa Simba Emanuel Okwi (nyuma) ni Kichuya.
Mchezo ukiendelea kaitaba John Bocco akigombea mpira wa kichwa na Mchezaji wa Kagera Sugar.

Beki wa Kagera Sugar Juma Nyosso akikimbiza mpira akiwa sambamba na mshambuliaji wa Kagera Sugar Emmanuel Okwi.

Kadi ya Njano ilitolewa kwa mchezaji wa Kagera Sugar Fakhi

Emmanuel Okwi akiwa Chini chaliii!!

Mshambuliaji wa Kagera Sugar akimwangalia Mwamuzi juu ya rafu aliyotendewa na Mchezaji wa Kagera Sukari.

Okwi akiwa chini

Mlinzi wa Kagera Sugar Asante Kwasi akijutia kukosa nafasi ya kufunga bao

John Bocco akiwa chini na mwezake wa Kagera Sugar baada ya patashika kutokea...kipindi cha pili. Picha zote na Faustine Ruta

Jukwaa kuu wakiutaza mchezo

Viongozi mbalimbali wakiwa jukwaa kuu wakiutaza mchezo Kagera sugar dhidi ya Timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam.


Hakuna kupita!! hapa!

Mchezaji wa Kagera Sugar alimdhibiti mchezaji wa Simba kupita hapa!

Kichuya akijiandaa kupiga kona.

Mavugo wakati huo akipiga jalamba
Wakisubiri mpira wa kona

Patashika kwenye lango la Kagera Sugar kipindi cha pili

Juma Kaseja akimcheki John Bocco

John Bocco akimtoka Mohamed Fakhi wa kagera Sugar

Baada ya kumtoka aliachia pasi kwa Mdemla aliyemalizia nyavuni na kuwanyanyua mashabiki wa Simba kwenye Viti kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Shangwe kwa Ndemla
Kapombe akiambaa na mpira kumsonga kipa wa Kagera sugar Juma Kaseja.


Wakipongezana kwa bao

Mashabiki wakishangilia nao wa Timu ya Simba baada ya kufunga bao
Raha kwa Mashabiki wa Simba.

Picha zote na Faustine Ruta wa Bukobasports.com

Mwinyi Vehicle(kushoto) akiwa na Mwinyi mwenzake (kulia) wakati wa Mtanange huo ukiendelea jioni ya leo, Simba Kashinda bao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Mashabiki wa Timu ya Simba leo wameingia kwa wingi kwenye Dimba la Kaitaba kuwapa sapoti wenzao wakati wa mchezo huo wa Kagera Sugar vs Simba SC.
Wachezaji wa Kagera Sugar baada ya mchezo kumalizika wakiwa wamepoteza mchezo huo wa bao 2-0 mbele ya timu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam.