Thursday, January 4, 2018

FULL TIME: MANCHESTER CITY 3 - 1 WATFORD

Timu ya Manchester City imeonyesha kutotetereka na kusitishwa kwa rekodi yao ya kushinda michezo 18 mfululizo ya Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya jana kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Watford.
Ikicheza zikiwa zimepita siku mbili tangu watoke sare tasa na Crystal Palace, City walipata goli lao kwa kwanza katika dakika 38 likiwa goli la mapema mno kupitia kwa Raheem Sterling akitumbukiza kimiani mpira wa krosi ya Leroy Sane.

Manchester City ilipata goli la pili baada ya Christian Kabasele kujifunga akijaribu kuokoa krosi ya Kevin de Bruyne, Sergio Aguero akafunga la tatu na kisha Andre Gray akafunga goli la kufutia machozi katika dakika za mwisho.
Raheem Sterling akifunga goli la kwanza la Manchester City, likiweka rekodi ya goli la kufungwa mapema mno katika msimu huu
Mshambuliaji Sergio Aguero akifunga goli la tatu la Manchester United