Monday, January 8, 2018

HARRY KANE NI BALAA ATUPIA BAO MBILI TOTTENHAM WAKIIBUKA NA USHINDI WA BAO 3-0 DHIDI YA AFC WIMBLEDON


Kocha Mauricio Pochettino amesema Harry Kane anaweza kubakia Tottenham katika muda wake wote wa kusakata soka baada ya jana kufunga magoli mawili na kuisaidia kupata ushindi dhidi ya Timu ya AFC Wimbledon.
Katika mchezo huo wa Kombe la FA raundi ya tatu Kane na Jan Vertonghen waliipatia Tottenham ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya timu hiyo ya AFC Wimbledon inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza.


Harry Kane akijipinda na kuachia shuti lililozaa goli kati ya magoli yake mawili aliyofunga

Mpira uliopigwa na Jan Vertonghen ukielekea kuja wavuni na kuandika goli la tatu la Tottenham