Thursday, January 4, 2018

HECTOR BELLERIN AIOKOA ARSENAL KATIKA DAKIKA ZA MAJERUHI, ASAWAZISHA NA KUUMALIZA 2-2 DHIDI YA BLUES


Hector Bellerin amefunga kwa shuti kali la dakika za mwisho na kuisaidia Arsenal kuambulia pointi katika mchezo wake wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Chelsea ulioishia kwa sare 2-2.
Pande zote mbili zilipata nafasi 33 za kufunga zilizodhibitiwa na makipa mashujaa wa mchezo huo Petr Cech wa Arsenal na Thibaut Courtois wa Chelsea waliyoruhusu magoli manne tu.

Katika mchezo huo Jack Wilshere alifunga goli la kwanza kwa Arsenal lakini Eden Hazard akasawazisha kwa penati dakika nne baadaye naye Marcos Alonso akaongeza la pili.


Mchezaji Marcos Alonso akifunga goli la pili la Chelsea

Mpira uliopigwa na Hector Bellerinukijaa wavuni na kuisawazishia Arsenal goli la pili