Monday, January 22, 2018

HENRIKH MKHITARYAN ATUA ARSENAL LEO HII, ATAMBULISHWA!

Arsenal have announced the signing of Manchester United midfielder Henrikh Mkhitaryan
Klabu ya Arsenal  imemsajili Henrikh Mkhitaryan  kutoka Manchester United  leo hii.

Mkhitaryan akiwa huko London Colney jioni hii jumatatu wakati wa kukamilisha usajili wake.
Mkhitaryan, mwenye umri wa miaka 28,ambaye ni raia wa Armenia amefanyiwa ukaguzi wa kimatibabu jana jumapili na leo hii Jumatatu kutua Emirates, huku Sanchez mwenye umri wa miaka 29 raia wa Chile alifanyiwa vipimo jana Juampili.

Muda wa mkataba wa Mkhitaryan na kitita atakachopokea kama mashahara hakijulikani.
Arsene Wenger awali alisema Sanchez atajiunga na United iwapo tu Mkhitaryan atahamia Arsenal.

Sanchez alikosa ushindi wa Arsenal wa mabao 4-1 dhidi ya Crystal Palace Jumamosi kwasababu alikuwa anasafiri kwenda Manchester.

"Huwezi kusafiri kwenda kaskazini na ucheze soka kwa wakati mmoja," alisema Wenger.