Wednesday, January 24, 2018

JOHN BOCCO AONGOZA KWA KUMFUNGA KIPA JUMA KASEJA!

John Bocco akimtoka mchezaji wa Kagera Sugar FakhiNahodha wa klabu ya Simba John Raphael Bocco ni moja ya wachezaji wakongwe nchini kwasasa kutokana na kucheza Ligi kuu Tanzania Bara kwa muda mrefu akiwa na kikosi cha Azam Fc kabla ya kutua Simba.
Bocco ambaye amekuwa ni mchezaji mwenye hatari zaidi kwasasa kunako klabu ya Simba Jumatatu aliisaidia timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya timu ya Kagera Sugar kwa mabao 2-0.

Mara baada ya kumfunga goli golikipa wa Kagera Juma Kaseja Bocco ameweka rekodi ya kumfunga Golikipa huyo mabao 10 na kuwa ni mshambuliaji pekee wa Tanzania aliyewahi kufanya hivyo.

Bocco amekuwa akimfunga Kaseja toka akiwa klabu ya Simba wakati huo Bocco akiitumikia Azam Fc na mara nyingi ndiye mchezaji pekee ambaye anamuumiza kichwa Juma Kaseja kutokana na kumfunga mara nyingi.

Jumatatu aliisaidia Simba kuondoka na alama tatu kwa bao la dakika ya 79 kwa pasi safi ya Sbomari Kapombe baada ya Saidi Ndemla kuifungia Simba bao la kwanza dakika ya 72.

Mbali na mchezo huo Singida wakiwa ugenini mkoani Ruvuma wamelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Majimaji Fc bao la Singida likifungwa na Papy Kambale dk 28 kabla ya winga hatari wa majimaji Peter Mapunda kuisawazishia Majimaji dakika ya 85 na kufanya matokeo kuwa 1-1