Wednesday, January 17, 2018

JOSE MOURINHO NA MAN UNITED WAKARIBIA KUAFIKIANA KUHUSU MKATABA

Klabu ya Manchester United inakaribia kufikia makubaliano na kocha wake Jose Mourinho wa kuongeza mkataba mpya.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yanaendelea vyema na ni suala la muda tu kabla ya Mourinho hajaongeza mkataba mpya klabuni hapo na mkataba wake wa sasa unafikia ukingoni mwaka 2019.
Taarifa za ndani ya klabu zinaeleza kuwa kama kocha huyo atasaini mkataba mpya utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2021.

Licha ya kulaumiwa na wachambuzi wengi wa soka pamoja na washabiki wa klabu ya Man kuwa timu hiyo inacheza mchezo wa kujilinda bado viongozi wa United wanaona kuwa Mourinho anaweza ibeba timu hiyo katika kuipa mataji makubwa barani Ulaya.
Image result for jose mourinhoMourinho alijiunga na United mwaka 2016 kuchukua mikoba ya Luis Van Gaal, ameisadia Man United kutwaa ubingwa wa kombe la Europa na Lile la EfL Carabao.