Monday, January 22, 2018

JUMA NYOSSO ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI BAADA KUMPIGA SHABIKI!Beki wa Kagera Sugar Juma Nyosso amekamatwa na Polisi baada ya kumpiga shabiki hadi kuzimia baada ya mchezo wa Kagera Sugar vs Simba uliyomalizika kwa Simba kupata ushindi wa magoli 2-0 mjini Kagera

Beki wa Kagera Sugar Juma Nyosso amejikuta akitiwa mbaroni na polisi mjini Bukoba kwa madai ya kumtwanga shabiki ngumi mara baada ya mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Kagera Sugar kupigwa 2-0 na Simba SC kwenye dimba la Kaitaba.

Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya mpira kumalizika wachezaji wa Kagera Sugar walikuwa wanakwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo (dressing-room) ambapo inadaiwa kuwa baadhi ya mashabiki wanaoaminika kuwa ni wa Kagera Sugar wakawa wanawarushia maneno makali (matusi) wachezaji hao.

 Kufuatia maneno hayo, Nyosso alionekana kukosa uvumilivu na kuamua kumtwanga ngumi mmoja wa mashabiki hao ambaye alizimia papo hapo.

Gari ya wagonjwa (ambulance) ilifika na kumchukua majeruhi na kumkimbiza hospitali na dakika chache baadaye polisi walikwenda kumchukua Nyosso na kwenda naye kituo cha polisi.

Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitafuata baadaye