Thursday, January 18, 2018

KELECHI IHEANACHO AWEKA REKODI YA GOLI LA UAMUZI WA TEKNOLOJIA YA VIDEO


Mshambuliaji mwenye asili ya Nigeria Kelechi Iheanacho amekuwa mchezaji wa kwanza katika soka la Uingereza kufunga kwa msaada wa uamuzi wa video wakati Leicester City ikiifunga Fleetwood magoli 2-0 katika mchezo wa raundi ya tatu wa kombe la FA.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City alifunga goli la kwanza baada ya kunasa pande kutoka kwa Islam Slimani, lakini goli lake la pili ndilo lililoivua uamuzi wa kutumika video.

Refa Jonathan Moss alikubaliana na muamuzi aliyetumia video Mike Jones, ambaye alimuambia kuwa guu la Nathan Pond lilimfanya Iheanacho asiwe tena ameotea, na goli hilo kukubaliwa baada ya sekunde 67 kupita tangu kufungwa.


Kelechi Iheanacho akifunga goli lililoibua utata na kuamuliwa kwa video

Refa Jonathan Moss akisikiliza maamuzi kutoka kwa refa msaidizi anayetumia video