Monday, January 22, 2018

FULL TIME: KAGERA SUGAR 0 vs 2 SIMBA SC, NDEMLA NA BOCCO WALIPA KISASI KAITABA LEO, SIMBA AREJEA KILELENI!

Kipindi cha pili dakika ya 70 Said Ndemla aliipatia Simba goli la Kwanza na kufanya Simba kuongoza kwa bao 1-0. Wakati huo baaada ya bao hilo Shomari Kapombe aliingia kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe Simba akichukua namba ya Gyan.
Kipindi hicho cha pili dakika ya 80 John Bocco aliipachikia Simba bao la pili Baada ya kazi nzuri ya Shomari Kapombe aliyeingia kipindi hicho cha pili na Simba kuwatandika bao la pili na Simba kuongoza bao 2-0' Hadi dakika 90 zinamalizika Simba 2-0 Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Ushindi huo unawarudisha Simba kileleni wakiwa na pointi 32.

Kapombe akipongezana na Emanuel Okwi (nyuma) ni Kichuya