Monday, January 22, 2018

FULL TIME: EPL - SWANSEA CITY 1 vs 0 LIVERPOOL

Swansea 1 - 0 Liverpool (Alfie Mawson, dakika ya 40)
Liverpool na Swansea zimekutana na tukashuhudia Liverpool aliyemtandika Man City wiki iliyopita nae akitunguliwa bao 1-0.
Mlinda mlango wa Liverpool  Lois Karius hakuweza kabisa kudaka mpira wa  Mawson (kulia) ambao ulipigwa ukitokea kama kona. Van Dijk akishangilia bao
Mawson akishangilia bao lake na wenzake kwenye uwanja wao wa nyumbani baada ya kuifunga liverpool bao 1-0 dakika ya 40 na bao hilo kudumu hadi dakika ya 90. Swansea City wako nafasi ya mkiani na ushindi huo haukuwatoa huko chini bali waliongeza pointi na kufikia 20 tu. 
Mchezaji bora katika mchezo huo Lukasz Fabianski kipa wa Swansea ambaye alilinda lango lake thabiti na kuumaliza bila kufungwa bao.