Monday, January 22, 2018

MANCHESTER UNITED WAMTAMBULISHA ALEXIS SANCHEZ OLD TRAFFORD LEO HII JUMATATU JIONI, HENRIKH MKHITARYAN NAE ATUA EMIRATES LEO HII!


Sanchez  Manchester United
Sanchez amesaini  UnitedManchester United wamemtambulisha Alexis Sanchez leo hii jumatatu jioni kwenye Uwanja wa Old Trafford akitokea Arsenal, huku uhamisho wake ukiambatana na mchezaji wa Man United kwenda Arsenal Henrikh Mkhitaryan ambaye walikuwa wakimhitaji tangu msimu uliopita.
Timu hiyo ya Mashetani wekundu iliipiku Arsenal kumsajili Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund mnamo July 2016 kwa kima cha £ milioni 26.3.

United's newest player putting pen to paper on his contract with the Old Trafford sideSanchez, amefunga mabao 80 katika mechi 166 za mashindano yote akiichezea Arsenal tangu kusajiliwa kutoka Barcelona mnamo July 2014 kwa £ milioni 35.
Video imethibitisha kuwa Sanchez atavaa jezi namba 7

Raia huyo wa Chile ambaye mkataba wake na Arsenal ulitarajiwa kumalizika msimu wa joto mwaka huu alitarajiwa kusajiliwa Manchester City mwaka jana.
Imeabinika wiki hii kwamba City iliamua kutomsajili tena.

Sanchez akiucheki uwanja wa Old Trafford.


Mambo safi!!!

Klabu ya Arsenal pia imemwanika Henrikh Mkhitaryan.Mkhitaryan juggling a ball during his unveiling at Arsenal's London Colney on Monday