Monday, January 22, 2018

MASHABIKI WA KIKUNDI CHA "SIMBA KWANZA" WAMTUNUKU NDEMLA KITITA BAADA YA KUWA MCHEZAJI BORA WA MECHI YA KAGERA SUGAR vs SIMBA SC BAADA YA MCHEZO KUMALIZIKA.

Kiungo wa Simba Hamis Said Juma (Ndemla) amepokea kitita baada ya mchezo kumalizika jioni ya leo Simba ikiibuka kidedea kwa goli 2-0 dhidi ya Timu ya Kagera Suagr. Mashabiki hao wa Kundi la "Simba  Kwanza" wenye makazi yao Sinza jijini Dar es Salaam wamefurahia baada ya Timu yao kushinda bao 2-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Ndemla amekuwa Mchezaji bora kwenye mchezo huo. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Kipande cha mkundu wa Ndizi nacho kilionekana wakati wa kumtunuku Ndemla fedha hizo kwenye maeneo ya Uwanja wa Kaitaba mara baada ya mchezo huo kumalizika.