Saturday, January 13, 2018

MESSI AFUNGA MAWILI BARCA IKITINGA ROBO FAINALI YA KOMBE LA COPA DEL REY

Lionel Messi amefunga mara mbili katika dakika 15 za mwanzo wakati Barcelona ikiichakaza Celta Vigo na kutinga robo fainali ya kombe la Copa del Rey.
Barcelona ilidhamiria kupata ushindi katika mchezo huo baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza, ambapo ilishusha kikosi kilichokamilika safari hii.
Messi alifunga magoli hayo akipatiwa pande na Jordi Alba, kisha Alba akafunga magoli mengine yakafungwa na Luis Suarez pamoja na Ivan Rakitic.


Lionel Messi akifunga goli lake la pili baada ya kupata pande la Jordi Alba

Ivan Rakitic akiwa ameupiga mpira kwa kichwa uliozaa goli la tano la Barcelona