Wednesday, January 24, 2018

MJERUMANI ANGELIQUE KERBER ATINGA NUSU FAINALI AUSTRALIA OPEN


Bingwa mara mbili wa Grand Slam Angelique Kerber amemchakaza Madison Keys katika dakika 51 na kutinga nusu fainali ya Australia Open.
Mjerumani huyo mwenye miaka 30 alikuwa katika kiwango bora akimfunga Mmarekani Keys kwa seti 6-1 6-2 katika dimba la Rod Laver Arena.
Keys, ambaye alitinga fainali za mwaka 2017, alihaha mno muda wote wa mchezo huo na kupata pointi 18 kati ay 46 wakati akianzisha mpira.


Mwanadada Angelique Kerber akipambana kurejesha mpira katika mchezo huo

Mmarekani Keys akimpongeza Angelique Kerber baada ya kuibuka mshindi