Monday, January 22, 2018

MKUU WA MKOA WA KAGERA MEJA JENERALI MSTAAFU SALUM MUSTAFA KIJUU AFURAHIA MPAMBANO WA SIMBA NA KAGERA SUGAR KAITABA LEO

Na Faustine Ruta, Bukoba
Simba imezidi kujichimbia kileleni baada ya kuichapa Kagera Sugar kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba hii leo jioni.
Bao za Simba Sc leo hii zimefungwa kipindi cha pili baada ya kumaliza dakika 45 timu zote mbili zikiwa 0-0. Bao la kwanza limefungwa na Said Ndemla na bao la pili limefungwa na John Bocco baada ya mabeki wa Kagera Sugar kujichanganya.
Kipindi cha pili dakika ya 70 Said Ndemla aliipatia Simba goli la Kwanza na kufanya Simba kuongoza kwa bao 1-0.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu akisalimia wachezaji wa Timu ya Simba muda mfupi kabla ya mtanange kuanza hii leo Kaitaba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu akisalimia waamuzi wa mtanange huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu akiwa sambamba na Salumu Umande Chama.Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu na Viongozi wengine wakiwa meza kuu wakifuatilia mtanange wa Kagera Sugar na Simba Sc.

Simba imerejea kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya kufikisha pointi 32.

Simba imerejea kileleni baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Ushindi wa leo unairejesha Simba kileleni baada ya kuwa imeporomoka hadi nafasi ya pili baada ya ushindi wa Azam FC iliyofikisha pointi 30.
Mabao ya Simba leo yamefungwa na Said Ndemla katika dakika ya 70 na John Bocco akamalizia kazi kwa kufunga bao la pili dakika ya 80.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu akitoa nasaha zake kabla ya Mchezo kuanza kati ya wenyeji Kagera Sugar dhidi ya Timu ya Simba Sc ya Jijini Dar es salaam.