Friday, January 5, 2018

MOHAMED SALAH MCHEZAJI BORA AFRIKA AMSHINDA MANE NA AUBAMEYANG


Mshambuliaji Mohamed Salah amempiku mchezaji mwenzake wa Liverpool Sadio Mane pamoja na mchezaji wa Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang na kutwaa tuzo mchezaji bora wa CAF wa Afrika.
Salah raia wa Misri mwenye umri wa miaka 25, amepata kura 625 zilizopigwa na makocha wa timu za taifa Afrika, makapteni wa timu pamoja na idadi ndogo ya waamuzi na waandishi waliochaguliwa.

Mohamed Salah ambaye kwa sasa yupo katika kiwango kizuri tangu ajiunge na Liverool katika msimu huu alifunga goli lililoipeleka Misri katika michuano ya kombe la dunia itakayofanyika Urusi.


Mohamed Salah akikabidhiwa tuzo ya CAF ya mchezaji bora Afrika 2017

Mohamed Salah, Sadio Mane pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang wakiwa katika picha ya pamoja