Saturday, January 13, 2018

MSHAMBULIAJI WA ARSENAL ALEXIS SANCHEZ KUONDOKA JANUARI, JE ATATUA MAN CITY AU MAN UNITED?


Mshambuliaji Alexis Sanchez ataondoka Arsenal Januari iwapo itatolewa ofa nzuri na kupatikana kwa mtu wa kuziba nafasi yake.
Ni dhahiri sasa wamiliki wa Arsenal wameanza kuridhia kimyakimya kuondoka kwa Sanchez kwa wiki kadhaa na sasa anaweza akaondoka baada ya kuitumikia klabu hiyo miaka mitatu na nusu.

Hata hivyo Arsenal wanasuasua kumuuza Sanchez bila ya kumpata mtu wa kuziba pengo lake, na kwa sasa rada zao zinalenga kumnasa Mshambuliaji Mbrazil wa Bordeaux Malcom.