Tuesday, January 23, 2018

NINI JUMA KASEJA ALICHOKISEMA BAADA YA KIPIGO CHA BAO 2-0 DHIDI YA SIMBA

Kipa namba moja wa Kagera Sugar, Juma Kaseja amesema wamefanya makosa ambayo yamewagharimu dhidi ya Simba.
Simba imerejea kileleni baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Kaseja amesema kikosi chao kilicheza vizuri lakini hawakuzitumia nafasi.

“Game plan yao imekuwa nzuri na wamefanikiwa kuyatumia makosa yetu mawiliw akafunga mabao mawili,” alisema.

“Lakini tumecheza vizuri na hatukuweza kuzitumia nafasi ambazo tulipata. Kikubwa sasa ni kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo.”

Inaonekana hali ya Kagera Sugar si nzuri kwa kuwa katika mechi 14 za Ligi Kuu Bara walizocheza, wameweza kukusanya pointi 12 tu. Juma Kaseja Mlinda mlango wa Kagera(kulia) akiwa pamoja na msemaji wa Timu ya Simba Sc mara baada ya mtanange wao kumalizika katika dimba la Kaitaba. Picha na Faustine Ruta, Bukoba