Wednesday, January 24, 2018

NMB YAINGIA MKATABA MWINGINE NA AZAM FC


Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Abdul Mohamed (kulia), akimkabidhi Mkurungezi Mkuu wa NMB, Imeko Bussemaker moja ya jezi zinazotumiwa na klabu hiyo msimu huu.

Klabu ya Azam FC imeendelea kuingia kwenye neema mpya baada ya kuingia tena mkataba mpya wa Benki ya wazalendo ya NMB.

NMB wanaonekana kufurahishwa na mambo yalivyokwenda katika mkataba wao wa kwanza na NMB baada ya kuonekana kuutendea haki mkataba wao wa awali wa benki hiyo hivyo imewaongezea mwingine wa mwaka mmoja ambao utawasaidia kupambana kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
Akizungumza wakati wa kusainishana mkataba huo Mkurungezi wa NMB, Imeko Bussemaker, alisema kwamba wameamua kuingia mkataba mpya na Azam FC.

Bosi huyo ameweka wazi namna ambavyo wamevutiwa na Azam FC na namna walivyoheshimu mkataba wao.
Wanaamini Azam itaongeza wigo mkubwa katika kuzalisha wachezaji wachanga hapa nchini ambao wataiinua hata timu ya taifa wanayoidhamini pia.
Naye, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohamed, yeye amewashukuru NMB kwa udhamini huo “Niwashukuru sana kwa hili lakini huku napenda niwaahidi kua siku chache zijazo nitarudi hapa tena kuwakabidhi Kombe la Ligi Kuu Bara.

"Kwani tunaamini hadi mwisho wa msimu mambo yatanyooka maana farsafa yetu kwa sasa tunaendelea kupambana kimyakimya kama tunamfukuza mwizi,” alisema Abdul.


Mkurungezi wa NMB,Imeko Bussemaker (kushoto),akikabidhi mkataba huo kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Abdul Mohamed ndani ya makao makuu ya ofisi hizo Posta jijini Dar es Salaam, mapema leo.

Nahodha wa timu ya Azam FC, Himidi Mao (kushoto), akimkabidhi kombe lao waliloshinda kwenye michuano ya mapinduzi Cup Mkurungezi Mkuu wa NMB,Imeko Bussemaker baada ya shughuli za kusainishana mkata mpya kumalizika.

Mkurungezi Mkuu wa NMB,Imeko Bussemaker (kushoto), akisaini mkata huo sambamba na Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Abdul Mohamed.

Baadhi ya wanahabari wakitekeleza wajibu wao wakati wa makabidhiano ya mkataba huo.

Wakurugezi na baadhi ya wafanyakazi wa NMB,wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiana mkataba huo.