Friday, January 5, 2018

SERENA WILLIAMS AJITOA MICHUANO YA WAZI YA AUSTRALIA

Mchezaji aliyewahi kushika nafasi ya kwanza katika tenesi duniani Serena Williams amejitoa katika michuano ya Wazi ya Australia inayofanyika mwezi huu huko Melbourne.
Serena raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 36, wiki iliyopita alicheza mechi yake ya kwanza tangu ajifungue mwezi Septemba.
Williams, mshindi wa Grand Slam mara 23 na bingwa mtetezi wa michuano ya wazi Australia, amesema ingawa yupo vyema, lakini hajafikia kiwango cha ubora wake anachokitaka.
Serena Williams akiwa na kombe lake alilolitwaa michuano iliyopita ya Wazi ya Australia
You might also like: