Wednesday, January 10, 2018

SERGIO AGUERO AIPA USHINDI MANCHESTER CITY DAKIKA ZA MAJERUHI


Sergio Aguero amefunga goli la ushindi dakika za majeruhi na kuisaidia Manchester City kutokea nyuma na kuishinda Bristol City kwa magoli 2-1 katika kombe la Carabao.
Kikosi cha Bristol City kilikuwa katika kiwango kizuri, hususan katika nusu ya kwanza na ilijikuta ikiongoza kwa goli la penati la Bobby Reid.
Laikini Kevin de Bruyne aliisawazishia Manchester City goli baada ya kugongeana vizuri na Raheem Sterling, katika mchezo huo wa nusu fainali uliokuwa na ushindani mkali.

Kevin de Bruyne akifunga goli la kusawazisha baada ya kugongeana vyema na Raheem Sterling

Sergio Aguero akifunga kwa kichwa goli la ushindi la Manchester City